Kimbunga Hidaya kushuhudiwa mwambao wa Pwani

  • | Citizen TV
    3,461 views

    Idara ya utabiri wa hali ya anga nchini imetoa tahadhari ya upepo mkali na kimbunga kwa watu wanaoishi maeneo ya Pwani ya Kenya kuanzia leo hadi jumatatu ijayo. Kwa mujibu wa idara hii, eneo la mwambao wa pwani litashuhudia mawimbi mazito baharini, kwenye hali iliyochangiwa na kimbunga kinachofahamika kama Hidaya ambacho kimeanza kushuhudiwa katika visiwa vya Comoros. Kimbunga hicho kinatarajiwa kuongeza maradufu viwango vya mvua. Aidha, Katika muda wa saa 24, maeneo kama Ziwa Victoria, Bonde la ufa, magharibi na mashariki mwa nyanda za juu za bonde la ufa pamoja na Nairobi zitashuhudia makali ya hali ya hewa kuanzia leo hadi tarehe tano mwezi huu. Mvua kubwa zinatarajiwa kuathiri kaunti arobaini na mbili nchini. Sasa Wananchi wametakiwa kuchukua tahadhari kutokana na kushuhudiwa kwa mafuriko ya ghafla na hata ukungu kushuhudiwa maeneo mengine na kutatiza watu kuona. Taarifa hii imewasilishwa kwa Rais, baraza la mawaziri pamoja na idara zinazohusika na masuala ya mazingira, misitu na majanga.